Connect with us

Soka

Aussems Mbabe Wa Vpl

Kocha wa Simba sc Patrick Ausems ameonyesha ubabe baada ya kuisadia timu hiyo kuibuka na ushindi katika mechi nne za ligi kuu ilizocheza mpaka sasa ambapo kufuatia ushindi huo mfululizo amepata tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba.

Mbeligiji huyo alioongoza Simba sc katika mechi tatu za mwezi septemba ambapo Kati ya michezo  hiyo mmoja nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar na miwili ugenini mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar na mabao 2-0 dhidi ya Biashara United na kuifanyaSimba kumaliza mwezi ikiwa nafasi ya kwanza.

Kocha huyo amewafunika Mohammed Rishard wa Prisons na Abdallah Mohammed Baresi wa JKT Tanzania ambapo ameshinda michezo yote huku Baresi  aliingoza JKT Tanzania kushinda michezo miwili, sare moja na kupoteza mmoja wakati Richard akifanikiwa kuiongoza Prisons kushinda michezo miwili na kutoa sare mmoja, ambapo ilishinda nyumbani mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, kisha ikashinda ugenini mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa na ikatoka sare ugenini na Lipuli ya mabao 2-2.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka