Connect with us

Soka

Aussems Kama Kawa

Licha ya kuzagaa kwa tetesi za kusitishiwa ajira yake kunako klabu ya Simba sc kocha Patrick Aussems ameendelea kuinoa timu hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika kesho jumamosi.

Awali Aussems aliondoka ghafla kwenda nje ya nchi huku taarifa zikidai alikua na matatizo ya familia japo kwa mujibu wa vyanzo vya ndani vinadai kocha huyo alikwenda kufanya usaili katika moja ya vilabu barani Afrika.

Simba inakabiliwa na mchezo huo mgumu siku ya kesho huku wakihitaji pointi tatu ili kutanua pengo la alama ambapo wamecheza jumla ya michezo tisa na kuambulia pointi 22 wakishinda michezo saba huku mmoja wakisuluhu na mmoja wakipoteza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka