Connect with us

Soka

Aussems Akalia Kuti Kavu

Imeelezwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Simba sc Patrick Aussems amepewa onyo na uongozi wa klabu hiyo kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo ambao haujawaridhisha viongozi na mashabiki wa klabu hiyo.

Chanzo chetu kutoka ndani ya klabu hiyo kinaeleza kwamba kocha huyo amekua na urafiki na baadhi ya mastaa katika timu hiyo kiasi cha kuleta masihala katika kazi.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema, Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji ameambiwa apunguze urafiki na wachezaji ili kufanikisha malengo yake.

Inaelezwa kuwa Aussems amekuwa na urafiki zaidi na wachezaji wa Simba kiasi cha kwamba kitendi hicho kinapelekea ashindwe kutimiza majukumu yake kisawasawa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka