Connect with us

Soka

‘Anastahili Adhabu’ Karia amfungukia Mwakalebela

Rais wa shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia amesema kwamba adhabu za kufungia watu zinasaidia kwa kiasi kikubwa na zitaendelea kulingana na kanuni na sheria zinavyosema.
“mkitaka tufanye mnavyotaka ninyi tutarudi kule, itakuwa utawala wa kambale kila mtu ana ndefu……wataendelea kufungiwa, mkiona nimewaonea (Karia amewafungia watu sana) nendeni mkanishtaki maadili”Alisema
Kuhusu Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club Fredrick Mwakalebela, Karia amesema Mwakalebela alitakiwa ‘apewe adhabu kali zaidi’ kwa sababu alihusika kwenye kupitisha sheria zinazotumika sasa pale Tanzania Football Federation hivyo anazijua vyema.
“ … kwa sababu ni Makamu Mwenyekiti Yanga?……uende ukaongee kwenye vyombo vya habari halafu uje useme ni utani?…” aliongeza Karia.

 

Cc:Viwanjani Leo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka