Connect with us

Soka

Alliance,Malale Hamsini Washindwana

Klabu ya soka ya Alliance ya jijini Mwanza imeachana na kocha Malale Hamsini baada ya mkataba wa kocha huyo kufikia tamati na pande mbili kushindwa kuafikiana kuhusu mkataba mpya.

Awali Alliance walikua na mpango wa kumuongezea mkataba kocha huyo lakini baada ya pande mbili kukutana walishindwa kufikia muafaka hasa katika suala la maslahi hali iliyosababisha kocha huyo kuamua kuachana na timu hiyo iliyochini ya Meya wa jiji la Mwanza James Bwire.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inaeleza kuwa ndani ya wiki hii benchi jipya la ufundi la klabu hiyo litatangazwa rasmi huku tarehe ya kuanza mazoezi na mahali rasmi pa kufanyia mazoezi haya vitatangazwa baadae huku zoezi la usajili likiendelea klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka