Connect with us

Soka

Alliance,Billo Mambo Safi

Timu ya Alliance Fc imefikia makubaliano na kocha Athuman Bilali “Bilo”kuifundisha timu hiyo kwa kumpa mkataba wa miaka miwili ili kuongoza benchi la ufundi la timu hiyo yenye makazi yake Ilemela Jijini Mwanza.

Billo akiwa na wachezaji wa Stand united enzi akiifundisha.

Billo aliyekua kocha wa timu ya Stand United iliyoshuka daraja sasa ataungana na Kessy Mzirai na Dadi Gilbert pamoja na kocha wa makipa Hussein Tade kuingoza timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu baada ya kocha Malale Hamsini kushindwa kufikia makubaliano na uongozi wa timu kuhusu kuongeza mkataba.

Awali uongozi wa Alliance  ulipanga kumuongezea mkataba Malale Hamsini huku Billo angechukua majukumu ya kocha msaidizi lakini baada ya kushindwana na kocha huyo aliyeiongoza Alliance kucheza michezo 13 katika uwanja wa Nyamagana pasipo kupoteza hata mmoja.

Yussuph Budodi,Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo alisema lengo la kuwakabidhi timu makocha wote wazawa watokea wa kanda ya ziwa ni kujaza uzalendo kikosini hapo.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka