Connect with us

Soka

Alliance Wapaa Kenya

Timu ya soka ya Alliance Fc imeondoka jijini Mwanza kwenda nchini Kenya kwa mwaliko maalumu wa kucheza mechi za kirafiki kujiweka sawa na ligi kuu inayoendelea nchini ambapo imesimama kupisha michuano ya kimataifa ya kalenda ya Fifa.

Ukizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo uongozi wa timu hiyo umesema safari hiyo ni mwaliko maalumu wa timu ya Gormahi Fc ambayo imeialika timu hiyo kushiriki mchezo huo huku ikiwaahidi kuwatafutia michezo mingine ya kirafiki ili kujiweka fiti zaidi.

Safari hiyo ya pia imewezeshwa na benki ya Access Bank ambao ni moja ya wadhamini wa klabu hiyo huku wadhamini wengine wakiwa ni kampuni ya Emirate Alluminium Profile.

Alliance inakabiliwa na mechi ngumu ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga sc baada ya mapumziko ya michuano ya kimataifa yatakapomalizika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka