Ni kama zali la mentali kwa mshambuliaji Ibrahimu Ajibu baada ya kusota akiwa jangwani na sasa anakula raha katika hoteli aliyokaa staa wa Uingereza Wayne Rooney akiwa na mastaa wenzake wa Simba sc.
Iko hivi,Simba imeweka kambi nchini Afrika ya kusini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa na kambi hiyo imewekwa katika mji wa Rustenburg ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ambapo katika hoteli waliyofikia mastaa wa klabu hiyo ni hoteli ambayo ilitumiwa na mastaa wa timu ya taifa ya Uingereza katika fainali za kombe la dunia 2010 nchini humo.
sehemu ya chumba cha kulala
Hoteli hiyo inayoitwa Royal Marang Hotel ipo ndani ya kambi ya michezo inayoitwa Bafokeng(Bafokeing sports campus) ambayo ina kila aina ya vifaa vya kisasa vya michezo yote maarufu duniani ikiwemo Gym za kisasa na viwanja vya soka,tenisi,kikapu,gofu,mpira wa ufukweni,uwanja wa riadha na vingine vingi huko soka pekee likiwa na viwanja visivyopungua sita.
Ajibu akiwa ndani ya Gym
ya kisasa iliyopo katika eneo hilo.
sehemu ya nje yenye bwawa la kuogelea
Ndani ya kambi hiyo kuna hoteli mbili zenye hadhi ya nyota tano na hoteli za kawaida zenye hadhi ya nyota mbili huku kukiwa na chumba cha matibabu ya uhakika na klabu ya wachezaji kwa ajili ya kucheza michezo ya kutiliza akili kama puli(pooltable) na michezo mingine.
Moja ya viwanja vya mazoezi vilivyopo katika eneo la hoteli hiyo ambapo wanaonekana wachezaji wa simba wakifanya mazoezi.
Hoteli hiyo ya kifahari ipo umbali wa lisaa kutoka mji wa Pretoria na nusu zaidi ukitokea Johanesburg nchini humo na hutumiwa na timu ambazo huweka kambi katika eneo hilo na Rusterburg na inakadiriwa Simba itatumia zaidi ya milioni 300 katika kambi hiyo nchini humo.