Connect with us

Soka

Ajibu atua Chamazi

Kiungo mshambuliaji wa Simba sc IbrahimAjibu Migomba amejiunga na matajiri wa Jiji la Dar es salaam Azam Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia waoka mikate hao wa Chamazi.

Taarifa kupitia ukurasa rasmi wa klabu ya Simba wa Instagram iliandika ”Kwa maslahi ya pande zote mbili, uongozi wa klabu umefikia makubaliano na mchezaji Ibrahim Ajibu kusitisha mkataba wake kuanzia leo Alhamisi Desemba 30, 2021.

Kipekee tunamshukuru Ajibu kwa namna alivyojitoa kupambana kwa ajili ya Simba, na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake. ”#NguvuMoja

Ajibu amcecheza kwa mafanikio makubwa kwenye klabu ya Simba akitwaa mataji mawili ya ligi kuu soka Tanzania Bara,mawili ya kombe la shirikisho la Azam,ngao mbili za jamii na kombe la simba.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka