Connect with us

Soka

Ajibu Alamba 100m Simba

Simba sc tayari imeshamalizana na Mshambuliaji Ibrahim Ajibu na muda wowote anaweza kutambulishwa rasmi baada ya mkataba wake na Yanga sc kufika tamati hivi leo june 30.

Inadaiwa kuwa iliwalazimu Simba sc kutoa kiasi kikubwa cha fedha ili kumnasa mshambuliaji huyo ambapo kiasi cha fedha milioni 80 pamoja na gari yenye thamani ya milioni 20 ndivyo walivyokubaliana na kumlainisha staa huyo aliyeongoza kwa kusaidia upatikanaji wa mabao 16 katika klabu ya Yanga sc.

Ajibu alikulia katika klabu ya Simba sc kabla ya kuondoka na kujiunga na watani zao ambapo msimu huu baada ya tetesi za muda mrefu zikihusisha kubaki Yanga au kwenda msimbazi ambapo sasa imefahamika kuwa msimu ujao atarudi katika klabu yake ya zamani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka