Connect with us

Soka

Acheni Uzushi-Zahera

Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera amekana tetesi zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusisha kurejea Yanga

Zahera aliyeweka makazi yake nchini, amesema hakuwasiliana na kiongozi yeyote wa Yanga kuhusu jambo hilo

Mcongomani huyo amesema walioanzisha uvumi huo wana lengo la kumgombanisha na waajiri wake hao wa zamani

“Sio kweli, sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga.. wanaandika Yanga wameniita tujadiliane ni waongo hakuna jambo hilo, amesema”

“Wanaoandika uongo huo hawana nia nzuri na mimi pamoja na klabu ya Yanga, nawaambia waache kufanya hivyo”

Tangu mkataba wake uvunjwe mwezi Novemba 2019, Zahera ameendelea kubaki nchini ambapo amebainisha kuwa licha ya kupokea ofa kutoka klabu kadhaa, bado hajafanya maamuzi

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka