Connect with us

Soka

AC na Inter kujenga Cathedral

Vilabu vya AC Milan na Inter Milan vinavyotumia uwanja wa Sansiro vimezindua mpango wa ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa utakaotumiwa na vilabu vyote viwili katika mashindano mbalimbali vitakavyoshiriki.

Uwanja huo utaitwa ‘The Cathedral’ utaenda kuchukua nafasi ya uwanja wa Sansiro unaotarajiwa kuvunjwa na mamlaka ya mji wa Milan na tayari umpangwa kujengwa ofisi za mji huo.

Mradi huo utachukua square mita za mraba 50,00o kwaajili ya michezo na burudani mbalimbali.Mji maalumu utajengwa kuuzunguka uwanja huo utakaokuwa na parking ya magari ya chini utakuwa pia na miundombinu ya michezo mingine na unatarajiwa kutengeza ajira za kutosha pia kuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya mji.Utekelezaji wa mradi huo unatajwa kukamilika mwaka 2027.

Rais wa AC Milan Pablo Scaroni amesema ”San Siro mpya utakuwa uwanja unaovutia zaidi duniani kwa jinsi ulivyobuniwa na muonekano wake kwa ujumla utakavyokuwa.Pia utachangia sana maendeleo ya vilabu vyetu katika ushindani.

Naye mtendaji mkuu wa Inter Allesandro Antonello amesema ”San Siro mpya utakuwa na mandhari ya kijani kizuri kipindi chote cha mwaka na itakuwa bustani ya watu wa Milan.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka