Klabu ya AC Milan imeanza mazungumzo na Manchester united kuhusu kumsajili mlinzi wa kati kutoka Ivory Coast Eric Bailly katika dirisha hili dogo la usajili la majira ya baridi barani Ulaya.
Kitasa huyo kwasasa yupo na timu yake ya Taifa ya Ivory Coast katika mashindano ya AFCON 2021 nchini Cameroon ambapo hii leo wanashuka dimbani kucheza dhidi ya Guinea ya Ikweta.
AC Milan wanahitaji beki wa kati kwa haraka kutokana na kuumia kwa beki wao Mdenmark Simon Kjaer ambaye atakuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki cha msimu.Timu hiyo inabakiwa na mabeki Fikayo Tomori na Nahodha Romagnoli lakini rekodi mbaya ya majeruhi kwa mabeki hao ndio kinachowafanya mabingwa hao mara saba wa kombe la Ulaya kuhitaji mlinzi mwingine mwenye uzoefu.
Alipotua Manchester united Bailly alionekana angekuwa mhimili mkubwa ndani ya timu hiyo lakini mambo yamebadilika baada ya kupoteza nafasi kikosini licha kuonesha uwezo mkubwa kila anapopata nafasi ya kuanza.
Kinachosubiriwa kwasasa ni AC Milan kutum ofa rasmi kwa mashetani wekundu ambao hata hivyo itakuwa vigumu kwao kumuachia beki huyo kutokana na wengi wa mabeki wake kuandamwa sana na majeruhi siku za hivi karibuni.Hata hivyo mchezaji mwenyewe kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali amekubali kwenda kuanza maisha mapya ndani ya Jiji la Milan.