Connect with us

Soka

Molinga Ruksa Kuwavaa Pyramids

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limewatoa hofu viongozi wa klabu ya Yanga kuwa wataruhusiwa kuwatumia wachezaji wao David Molinga na Mustafa Suleyman kwenye mchezo wa mtoano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc

Baada ya kuchelewa kupata vibali vya wachezaji hao, Uongozi wa Yanga uliiandikia barua CAF kutaka ufafanuzi wa suala hilo

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Rodgers Gumbo amesema CAF wamejibu barua hiyo ambapo wamewahakikishia kuwa wachezaji hao wataruhusiwa kucheza mechi ya Oktoba 27 na leseni zao zitatumwa kabla ya mchezo huo

Molinga amekuwa katika kiwango kizuri cha kupachika mabao, anaweza kuongeza makali ya safu ya ushambuliaji kwenye mchezo huo

Aidha bado haijafahamika kama mkongwe Kelvin Yondani atapona majeraha kwa wakati na kuwahi mechi hiyo itakayopigwa Jumapili Oktoba 27 huku beki  Lamine ambaye alionyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United nchini Zambia anaweza kukosa mchezo huo hivyo Mustafa Suleyman anaweza kuwa mbadala wake.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka