Connect with us

Soka

Ngoma Aibukia kwa Ndanda

Mshambuliaji wa Azam fc Donald Ngoma leo ameisaidia klabu yake ya Azam fc kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya ndanda fc katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex uliopo chamazi jijini Dar es salaam.

Ngoma aliiandikia Azam bao la kwanza dakika ya 33’ baada ya mabeki wa Ndada kuijchanganya na kumrahishia mshambuliaji huyo raia wa Zimbabwe aliyesajiliwa akitokea klabu ya Yanga sc iliyomtema baada ya kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Licha ya Ndanda kujitahidi kutafuta bao la kusawazisha lakini bahati haikua kwao kwani kabla ya mapumziko walijikuta wakifungwa bao la pili kupitia kwa Daniel Amoaha dakika ya 45+2 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao hayo licha ya juhudi za timu zote mbili.

Azam iliyonahasira baada ya kufurushwa na Triangle Fc ya Zimbabwe katika michuano ya kombe la shirikisho itaendelea na ligi siku ya October 5 ambapo itawakaribisha Namungo fc katika uwanja huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka