Connect with us

Soka

200ml Kuwamaliza Simba sc

Kama kuna anaedhani Yanga inauchukulia poa mchezo dhidi ya watani zao Simba ambao utapigwa Jumapili, pole yake kwani mabingwa hao wa kihistoria wamejipanga kwelikweli kushinda mchezo huo.

Wadhamini wa klabu ya Yanga kampuni ya GSM wameahidi kutoa kitita cha Tsh Milioni 200 kama Yanga itashinda mchezo huo.

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema fedha hizo watakabidhiwa ‘taslim’ baada ya mchezo ingawa utaratibu wa makabidhiano utabadilika kutokana na wingi wake.

Aidha Nugaz amesema kuwa bado GSM wanaendeleza utaratibu wa kutoa bonas ya Tsh Milioni 10 kwa wachezaji pale timu inaposhinda ingawa kwa sasa hawatangazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka