Connect with us

Makala

Mdomo Wamponza Wilder

Bondia Tyson Furry amefanikiwa kumpiga bondia Deontay Wilder na kuchukua ubingwa wa dunia wa uzito wa juu katika pambano lililofanyika leo Las Vegas Marekani.

Pambano hilo lililotikisa dunia katika mizani ya uzito wa juu ambapo Furry alikua anasaka heshima baada ya kuhisi alidhulumiwa ushindi katika pambano la awali disemba mwaka 2018.

Furry alifanikiwa kumuangusha Wilder mapema raundi ya tatu tu licha ya bondia huyo kuanza kwa kasi na mpaka kufika raundi ya tano tayari Furry alianza kunusa ushindi baada ya kumuangusha tena Mmarekani huyo.

Pambano lilimalizika raundi ya saba baada ya timu ya Wilder kurusha taulo uwanjani kiashiria cha kukubali pambano liishe ili kumuokoa bondia wao baada ya kumuona amezidiwa na makonde.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala