Connect with us

Makala

Zlatiko Apewa Majukumu Mazito Yanga

Kocha mkuu mpya wa Yanga Sc,Zlatko Krmpotic amepewa majukumu makubwa kwenye mkataba wake ambayo anatakiwa kuyatekeleza katika msimu unaoanza leo Septemba 6.

Taarifa zinaeleza kuwa kwenye mkataba wa kocha huyo wa miaka miwili amewekewa malengo ya kuhakikisha anachukua mataji yote watakayopewa kushiriki liliwemo la ligi kuu bara na kombe la FA ambayo yote yanashikiliwa na watani wao wa jadi,Simba Sc.

Mserbia huyo ameanza kibarua cha kukinoa kikosi hicho kilichoweka kambi yake kwenye Kijiji cha Avic Town huko Kigamboni na leo anaanza kukaa benchi kwa mara ya kwanza wakati wachezaji wake wakicheza na Tanzania Prisons uwanja wa Mkapa jijini Dar-es-salaam.

Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa GSM wamechukua dhamana yote ya msimu wa pili ligi kuu bara na kusimamia usajili wote kwa kuchukua wachezaji waliokuwa bora ili kuhakikisha wanauchukua ubingwa wa ligi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala