Connect with us

Makala

Yikpe Na Molinga Wapata Sifa Kwa Mbelgiji

Kocha wa Yanga Luc Eymael amewachambua washambuliaji wake David Molinga na Yikpe Gnamein kuwa ni wenye uchezaji wa tofauti wawapo uwanjani.

Eymael ameiongoza Yanga kuibuka na ushindi katika michezo miwili mfululizo mmoja wa Ligi na mwingine wa Kombe la FA.

Alisema watu wamekuwa wakimbeza Yikpe lakini kwake   kwake ni mshambuliaji mzuri kwani kazi ya mshambuliaji ni kufunga na tulimuingiza katika mchezo wa Tanzania Prisons akafanya kazi.

Aliendelea kufafanua kwa kusema amekuwa akivutiwa na hesabu za mshambuliaji huyo katika kutafuta nafasi za kufunga.

Uchezaji wa Molinga ni tofauti na mshambuliaji mwenye uwezo wa kukaa na mpira mguuni kwani nguvu alizonazo zineweza kumsaidia kupita kwa wepesi katika msitu wa mabeki hata wakiwa watatu alisema Eymael.

Molinga ndiye kinara wa mabao Yanga akiwa amefunga magoli matano akifuatiwa na Patrick Sibomana mwenye mabao manne huku Yikpe tangu amejinga na Yanga amefunga mabao mawili moja upande wa Ligi na lingine katika kombe la FA.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala