Connect with us

Makala

Yanga,Gsm Wazidi Kunoga

Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka GSM Eng. Hersi Said amekiri kuwa tayari kampuni ya GSM wamesaini mkataba na klabu ya Yanga Sc kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za klabu (Club Merchandise) ambazo zitakuwa na chapa ya Yanga Sc.

Mkataba huo kati ya Yanga Sc na GSM utaipa fursa kampuni ya GSM kutumia chapa ya Yanga kutengeneza bidhaa nyingine tofauti na jezi. Bidhaa hizo ni kama truck suits, t-shirts, vikombe,saa, viatu , bracelets, na nyingine nyingi ambazo zitatengenezwa.

Eng. Hersi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kituo cha Azam Tv kupitia kipindi cha michezo cha Mshike Mshike Viwanjani.
Hii ni moja ya njia ambayo itaongeza mapato ya Klabu ya Yanga Sc kutokana na mauzo yatokanayo na bidhaa hizo zitakazo zalishwa na kampuni hiyo ambapo Mashabiki na Wanachama wa Yanga Sc wataweza kununua bidhaa hizo kuanzia msimu unao kuja (2021).

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala