Connect with us

Makala

Yanga Yapindua Benchi La Ufundi

Yanga Sc imeamua kuwaondoa wazawa wote katika benchi la ufundi na kubakiza raia wageni wawili kutoka Afrika Kusini mara baada ya kumpiga chini kocha mkuu,Luc Eymael kwa tuhuma za ubaguzi.

Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa Yanga,Dominick Albinius amesema kuwa baada ya kuwaondoa wachezaji wao 14 sasa wamefanya mabadiliko pia katika benchi la ufundi.

Aliongeza kwa kusema kuwa aliyekuwa kocha wao msaidizi wa kwanza,Charles Mkwasa amemaliza muda wake hivyo anahitaji kupumzika sambamba na kocha wa makipa ,Peter Manyika huku aliyekuwa meneja wa kikosi,Abeid Mziba na mtunza vifaa,Fred Mbuna wao wamebadilishiwa majukumu.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala