Connect with us

Makala

Yanga Ya Leo Ipo Hivi

Ofisa wa habari wa Yanga Sc ,Hassan Bumbuli amewaomba mashabiki wa Yanga Sc kujitokeza kwa wingi leo katika kuadhimisha kilele cha wiki ya wananchi ambayo itahitimishwa leo uwanja wa Benjamin Mkapa,Jijini Dar-es-salaam.

Maadhimisho hayo yanaifikisha Yanga Sc kuwa na miaka 85 tangu kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1935,hivyo katika kuhitimishwa kwake leo ,kikosi kipya cha msimu ujao wa ligi kuu bara na michuano mingine kitatambulishwa pamoja na jopo la benchi la ufundi.

Kocha mkuu wa Yanga Sc,Zlatiko Krmpotic ni miongoni mwa benchi la ufundi atakayetambulishwa leo baada ya kuwasili jana na kulazimika kwenda kuwaona vijana wake atakaofanya nao kazi wakifanya mazoezi wakijiandaa kuhitimisha siku yao.

Ndani ya Yanga Day pia kunatarajiwa kuwa na mwanamziki wa kizazi kipya ,Harmonize’Konde Boy’ ambaye atakuwepo kuwaburudisha wanajangwani hao katika kuadhimisha sikukuu ya kilele cha wananchi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala