Connect with us

Makala

Yanga Waituliza Alliance

Mabao ya Patrick Sibomana na David Molinga yalitosha kuipa ushindi Yanga katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Alliance uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba Mwanza.

Mabao ya dakika za 25 na 69 yalipatikana baada ya mabeki wa Alliance kufanya uzembe ambapo Waliruhusu Sibomana kupiga shuti kwa guu la kushoto huku pia wakimruhusu Kaseke kuingia na mpira kwenye boksi na kumpasia Molinga ambaye aligeuka na kufunga.

Alliance walipata bao la kufutia machozi kutokana na uzembe wa kipa Farouk Shikalo na mabeki wa Yanga waliomruhu Juma Nyangi kupiga shuti kali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala