Connect with us

Makala

Yanga Kukosa Milioni 40 GSM ni Kizaazaa

Timu ya wananachi Yanga Sc imekosa milioni 40 baada ya kukosa matokeo mazuri katika mechi nne mfululizo ambazo zote walitoka sare ikiwa ni kama ahadi ya GSM kuwapa milioni 10 katika kila mchezo endapo watapata ushindi.

Suala hili limebaki kuwaumiza wachezaji wa Yanga kwani inawapa nafasi finyu kuuchukua ubingwa ligi kuu ikiwa bado wapo nafasi ya nne huku Simba Sc ambao ni watani wa jadi wakiwa kileleni.

Niyonzima ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Yanga amesema kuwa kukosekana kwa milioni 40 imewapa changamoto kubwa sana kwani pesa hizo ndizo zinazotumika katika kutunza familia na yote kwasababu soka ndiyo kazi yao kuu inayoendesha familia zao.

“Ukweli sisi kama wachezaji tunapitia kipindi kigumu sana kwa sasa kwani soka ndiyo kazi yetu inayoendesha familia zetu, ikumbukwe kuna milioni 10 za mdhamini ambazo huwa tunapata ikitokea tumeshinda mchezo, michezo minne imepita hatujashinda, unaweza ukaona hapo tumekosa fedha kiasi gani”alisema Niyonzima

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala