Connect with us

Makala

Watatu Simba Kuikosa Ihefu Jumapili

Kocha mkuu wa Simba Sc,Sven Vandenbroeck amewachomoa nyota wake watatu ambao ni Luis Miqussone,Pascal Wawa na Chris Mugalo kwa kuwa hawakuwepo kwenye mazoezi ya awali na wachezaji wenzao kambini wiki mbili zilizopita.

Nyota hao watatu wanauwezekano mkubwa wa kuzikosa mechi mbili mfululizo baada ya kubakishwa Dar huku wanasoka wenzao wakiwa tayari wametua jijini Mbeya kujiandaa na mechi yao ya kwanza ya ligi kuu bara kwa msimu wa 2020/2021 dhidi ya Ihefu Jumapili,Septemba 6.

Kocha wa viungo,Adel Zrane amepewa jukumu kubwa la kuhakiksha wachezaji hao watatu wanakuwa fiti wakati wenzao wakiamsha popo katika mechi mbili za ugenini zitakazochezwa siku tofauti.

Wengine waliobakishwa Dar ni kipa namba tatu Ally Salim na Crypin Kipenye ambaye alikuwa anasubilia dili lake la kwenda kwa mkopo Ihefu msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala