Connect with us

Makala

Ufaransa Kimenuka,Amiens Wataka Haki Itendeke

Kikosi cha Amiens nchini Ufaransa nacho kimeanza mchakato wa kisheria dhidi ya maonevu baada ya kuteremshwa daraja kwenye ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) msimu huu huku Paris Saint-Germain (PSG) wakitangazwa mabingwa wa Ligue 1 kutokana na janga la Covid-19 .

Hadi hatua hiyo ilipochukuliwa, Amiens walikuwa wakishika nafasi ya 19 kwenye msimamo kwa alama nne zaidi nyuma ya Nimes huku pengo la pointi 10 likishika nafasi kati yao na Toulouse waliokuwa wakishika mkia huku zibakia mechi 10 pekee kwa kampeni za msimu huu kumalizika.

“Tutapigana kadri ya uwezo wetu kupinga maamuzi ya kibaguzi ambayo hayaonyeshi sifa nzuri za uanaspoti ambayo maamuzi hayo ni sawa na adhabu kwa Amiens na si haki pia si sawa,” alisema Mwenyekiti wa Amiens, Bernard Joannin .

Kwa upande wa wakili wa Amiens, Christophe Bertrand alisema “hatupingi kabisa maamuzi yaliyochukuliwa na wasimamizi wa soka ya Ufaransa kwa ushirikiano na serikali ila tunachopinga katika wasilisho letu rasmi kortini ni matokeo ya maamuzi hayo kwa mustakabali wa kikosi cha Amiens”.

Amiens wanawataka kubatilishwa kwa maamuzi ya kushusha daraja vikosi viwili kwenye Ligue 1 na badala yake kudumisha klabu zote zilizoshiriki kivumbi hicho muhula huu kisha kujumuishwa kwa Lorient na Lens ili kipute cha Ligue 1 msimu ujao wa 2020-21 kiwe na jumla ya timu 22 badala ya 20

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala