Connect with us

Makala

Tshishimbi Aweka Wazi Mkataba Simba

Nyota wa Yanga Sc,Papy Tshishimbi alitua jana Jangwani na kuteta na viongozi wake huku akiweka wazi mkwanja uliopo kwenye mkataba aliopewa na Simba ni shida.

Papy ameuweka mkataba huo nyumbani ukiwa na ofa nzuri atakazopewa endapo atakubali ,huku kocha Luc Eymael akisisitiza kuwa mchezaji huyo haondoki Jangwani.

Kiungo huyo mkataba wake kwa sasa umebaki miezi minne Jangwani lakini amewapa kipaumbele timu yake ya Yanga kwa vile amefanya nao kazi vizuri sana na tayari amefanya mazungumzo na bosi wa GSM ,Hersi Sadi na pia kukaa  na viongozi wake kwa muda wa dk 30 kabla ya kurejea kwake.

“Yanga nimeitumikia kwa miaka mitatu sasa ni lazima  niwe na heshima kwa klabu yangu ndo maana nimeanza kuwapa nafasi ya kuongea na mimi japo hatukumaliza hivyo nasubiri wiki kama mbili kutoka sasa kipi kitaendelea kwa kuwa sipendi kufanya maamuzi baada ya mkataba kumalizika kabisa”alisema papy

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala