Connect with us

Makala

TFF Yafafanua Pesa Za FIFA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebainisha kuwa fedha za maendeleo zitakazoletwa na FIFA ni kiasi cha dola 500,000 na hakitogawiwa kwa klabu za soka nchini kama ambavyo vimeomba katika siku za hivi karibuni.

TFF imesema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatolewa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kimichezo kama ilivyo katika utaratibu wa kutolewa kwake.

Pesa hii hutolewa kupitia programu iitwayo ‘FIFA Forward 2’. Ni kama mkataba ambao FIFA inakuwa imeingia na kila nchi yenye mwanachama wake juu ya matumizi ya fedha hizo na hazitakiwi kutumika nje ya hapo.

Ukienda kwenye ‘FIFA Forward 2’ kila mwanachama anapewa Dola 1 milioni ni karibu Sh 2.3 bilioni za kitanzania mwezi Januari na Julai ,ila wanapotoa Januari masharti  hayapo lakini lazima uwe umekidhi vigezo vya ukaguzi.

“Kwa Tanzania fedha hizi zinaitwa ‘operational cost’ ni fedha za uendeshaji wa shughuli za kimpira kwenye Programu za vijana, wanawake, mishahara ya makocha wa timu za taifa,na kwa sababu ni makubaliano, hivyo zinatumika kwa mujibu wa yale makubaliano,” alisema Kidao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala