Real Madrid iana matumaini ya kuishawishi Arsenal kumuachilia mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Star)
Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani amedokeza kuwa alijaribu kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 33 pamoja na mshambuliani wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye alijiunga na AC Milan, dirisha la uhamisho wa wachezaji lilipofunguliwa. (Mail)
Manchester United ipo tayari kumruhusu mlinzi wa England Chris Smalling kugeuza mkataba wake wa mkopo Roma kuwa wa kudumu, bora uwawezeshe kumpata mlinzi wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 28. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)
Arsenal pia imewasilisha ofa ya kumnunua Smalling dirisha la uhamisho litakapofunguliwa msimu wa joto, lakini Manchester United wanataka £25m. (Metro)
Mlinzi wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen, 32, amekiri kuwa hana uhakika anataka kusaini mkataba mpya utakamwezesha kusalia Spurs kwa msimu mwingine. (Mirror)
Arsenal inaamini watafanikiwa kuongeza mkataba mwingine wa mkopo na kiungo wa kati wa Real Madrid wa miaka 23-Mhipania Dani Ceballos endapo msimu huu utaendeleazaidi ya Juni 30. (Standard)
Leicester City imehusishwa na tetesi za uhamisho beki wa Atalanta Ubelgiji Timothy Castagne, 24. (Sport Foot, via Leicester Mercury)
Arsenal huenda wakamnyakua beki Mfaransa Dayot Upamecano kutoka RB Leipzig baada ya kiungo huy wa miaka 21 kuashiria anataka kuhama msimu huu wa joto. (Bild, via Star)
West Brom wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Croatia Filip Krovinovic, 24, kwa mkataba utakaogeuzwa kuwa wa kudumu baada ya mkopo wake kutoka Benfica utapomalizika. (Express and Star)
Chelsea imesitisha mazungumzo ya mkataba wa wachezaji kufuatia janga la coronavirus. Blues wana wachezaji wanne ambao mikataba yao ya sasa inaelekea malizika. Wanne hao ni -Willian, 31, Olivier Giroud, 33, Pedro, 32, na kipa wa Argentina Willy Caballero, 38. (Telegraph)
Barcelona wanatafakari uwezekano wa kuwapunguzia mshahara wachezaji wao wote kwa asilimia 70 hadi pale amri inayodhibiti matembezi nchini Uhispainia kutokana na janga la corona itakapoondolewa.(Guardian)
Klabu nane za Ligi ya Primia zimeungana kuizuia Manchester City kucheza Champions League msimu ujao kwa kutaka michuano hiyo isitishwe walipowasilisha rufaa dhidi ya marufuku ya miaka miwili waliowekewa na Uefa. (Times, subscription required)