Connect with us

Makala

Tetesi Za Usajili Ulaya

Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, 32, amepigiwa simu na klabu ya LA Galaxy kujadili uhamisho wa kuelekea Ligi ya Soka ya Marekani (MLS). (Express)

Messi amekiri kuwa anahisi kuna “mambo ya ajabu” yanaendelea Barcelona huku kukiwa na ripoti kuwa klabu hiyo ilikodi kampuni ya mitandao ya kijamii kukashifu wachezaji wake. (Mundo Deportivo, via Mail)

Hata hivyo, Messi yungali anaiona Barcelona kama nyumbani kwake licha ya tetesi za kutaka kuihama klabu hiyo. (ESPN)

Klabu ya Manchester United inaimani kuwa itamnasa mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 19, mwishoni mwa msimu, lakini kwanza itawapasa kufuzu kwa mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, amesema kuwa anajisikia fahari kuhusishwa na klabu ya Liverpoollakini anahisi kuwa huenda hayupo tayari kujiunga na klabu hiyo ambayo anasema ni “timu nzuri zaidi duniani.” (Metro)

Klabu ya Juventus imewaorodhesha mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus (22) pamoja na mshambuliaji wa Paris St-Germain na Argentina Mauro Icardi (27) kama kipaumbele katika dirisha l usajili la mwishoni mwa msimu. (Tuttosport – in Italian)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amesisitiza kuwa atacheza kwa moyo wote kwa Chelsea licha ya kushindwa kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi uliopita. (Mirror)

Klabu ya Arsenal inamnyatia beki wa Bayer Leverkusen Jonathan Tah, 24, ambaye anaweza kuondoka katika klabu yake kwa dau la euro milioni 40 mwishoni mwa msimu. (Bild – in German)

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala