Connect with us

Makala

Tetesi Za Soka Ulaya

Chelsea iko mbioni kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazil ,Philippe Coutinho ambaye anacheza kikosi cha Baryen Munich kwa  mkopo.

Tottenham watamlenga beki wa kati Issa Diop na mshambuliaji wa Wolves na Mexico,Raul Jimenez katika uhamisho wa gharama ya pauni milioni 96.9.

Wakala wa Jorginho amesema kuwa wataingia kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Chelsea baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa Raul Jimenez atamfuata kocha wa zamani Maurizio Sarri huko Juventus.

Mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Ujerumani ,Timo Werner anaweza kuwa anajiandaa kwa uhamisho kuelekea ligi kuu ya England kutokana na kuanza masomo ya lugha ya kiingereza ,huku Liverpool na Chelsea wakiwa wanamtaka mchezaji huyo.

Real Madrid wanajiandaa kumbakisha Gareth Bale kwenye msimu ujao pia wanajiandaa kutoa ofa ya mshambuliaji wa Serbia ,Luka Jovic kwenda Napoli likiwa ni jaribio la kushusha gharama ya pauni milioni 70 ya mchezaji wa miaka 24,Fabian Ruiz ambaye ananyemelewa na Manchester City.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala