Connect with us

Makala

Tarehe Za Vikao Vya Kurejesha Soka Uingereza

Zifuatazo ni tarehe muhimu katika juhudi za kurejesha soka la Uingereza katika kipindi hiki cha Janga la Covid-19, hiyo ni mara baada ya kikao cha jana kufanyika na vilabu vyote vya Uingereza ili kujua muafaka wa kurejea kwa ligi.

Jumatano, Mei 13 chama cha Wachezaji na chama cha Makocha wa vikosi vya EPL kushauriana na serikali kuhusu mikakati na taratibu mpya za afya .

Alhamisi, Mei 14 Mkutano kati ya viongozi wa chama cha wachezaji na chama cha makocha kujadili taratibu za afya zitakazokuwa zimetolewa na serikali pia katibu wa Utamaduni na viongozi wa soka la EPL watakuwa na kikao chao siku hiyohiyo kujadili suluhisho la serikali.

Jumatatu, Mei 18 Mkutano wa vikosi vyote vya EPL pia wachezaji wa EPL kurejea kambini kwa ajili ya mazoezi wakiwa makundini huku wakizingatia kanuni zote za afya zilizowekwa na wizara za afya na Serikali.

Jumatatu, Mei 25 mgawanyo wa wasimamizi wa soka la bara Ulaya (Uefa) kuhusu mipango ya kukamilishwa kwa ligi kuu za barani Ulaya msimu huu .

Jumatatu, Juni 1 Serikali kutoa taarifa ya mwisho kuhusu tarehe na mwafaka zaidi wa kurejeshwa kwa baadhi ya michezo bila ya mahudhurio ya mashabiki au kutolewa kwa taarifa rasmi ya kufutiliwa mbali kwa msimu huu mzima na kufichuliwa kwa yatokanayo na maamuzi hayo .

Ijumaa, Juni 12 Kurejeshwa kwa kipute cha EPL huku mchuano wa kwanza ukitandazwa bila mashabiki .

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala