Connect with us

Makala

Southampton Waitibulia Man Utd

Klabu ya Southampton imeharibu ndoto ya mashabiki wengi wa Manchester United ya kumaliza katika nafasi ya nne baada ya kusawazisha bao dakika za lala salama na kufanya matokeo ya mechi hiyo kuwa sare ya 2-2.

Southampton walikua wa kwanza kupata bao kupitia kwa Stuart Armstrong dakika ya 12 kisha Marcus Rashford akasawazisha dakika ya 20 na baadae Bruno Fernandes kumpa pasi ya mwisho Anthony Martial aliyefunga bao la pili dakika ya 23.

Wakati Mashabiki ya Man United wakitarajia mchezo kumalizika kwa matokeo hayo Michael Obafemi alisawazisha na kufanya mechi kumalizika 2-2 hivyo kuifanya Man United isalie nafasi ya tano ya msimamo kwa tofauti ya pointi moja na Chelsea mwenye pointi 60.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala