Connect with us

Makala

Sita Wasajiliwa Mbao Fc

Uongozi wa Mbao Fc wamefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji sita katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo lililofungwa juzi usiku.

Mwenyekiti wa kikosi hicho Solly Njashi alisema kuwa wamejipanga vyema katika kuhakikisha timu yao inafanya vizuri katika michezo ya ligi kuu  iliyobaki.

Waliosajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili ni Hussein Iddi kutoka Mtibwa Sugar Omary Wayne kutoka Friends Rangers na Wilson Wilson.

Mackyanda Franko kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miezi sita Hamis Mwinshehe kuttoka JKU ya Zanziabar kwa mkataba wa mwa mmoja na Paulo Maige kutoka Azam Fc kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha mkuu wa timu hiyo Hemedi Moroco amesema kuwa ana imani kubwa na wachezaji hao watasaidia kuinua kikosi na kukipa nguvu katika michezo ya ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala