Connect with us

Makala

Simba Yaahidi Kutolea Ufafanuzi Wa IST Ya Kabwili

Uongozi wa Simba Sc umeahidi leo kutolea ufafanuzi suala la  mlinda mlango wa Yanga Ramadhan Kabwili kudai kuwa aliahidiwa gari aina ya Toyota IST endapo angepewa kadi mbili za njano kweye mchezo wao wa msimu uliopita 2018/19.

Ofisa mkuu wa habari Simba Sc Haji Manara amesema kuwa watajibu tuhuma alizotoa mchezaji huyo ila cha msingi ajiandae kikamilifu na ushahidi wa tuhuma hizo.

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetoa  taarifa ya kusikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa si mpango mzuri kwa maendeleo ya soka na wameahidi kulifanyia uchunguzi kwa kujulisha vyombo vingine vya usalama ili viweze kubaini ukweli na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Cliford Ndimbo ambaye ni ofisa habari wa shirikisho la soka Tanzania amesema kuwa TFF siku zote imekuwa ikipiga vita vitendo vya upangaji matokeo katika mpira wa miguu na hivyo wanahidi kulifanyia uchunguzi wa kina swala hili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala