Connect with us

Makala

Simba sc Yaifanyia Umafia Yanga

Baada ya Awali kuifanyia umafia kwa Luis Miqquisone na Michael Sarpong klabu ya Simba sc imeifanyia umafia mwingine klabu ya Yanga baada ya kumsainisha beki wa pembeni wa Lipuli Fc David Kameta maarufu kama Duchu.

Awali Yanga iliripotiwa kumhitaji beki huyo na tayari ilianza mchakato wa kumsaninisha baada ya kocha Luc Eymael kumuhitaji lakini Simba imeingilia kati na kumsainisha beki huyo ikiwa na mapendekezo ya kocha Selemani Matola.

Taarifa zinadai Simba sc na Lipuli zimekubaliana na tayari mchezaji huyo amesaini mkataba wa awali wa miaka 3 na atatangazwa muda wa usajili ukifika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala