Connect with us

Makala

Shikalo,Moringa Kuwakosa Rollers

Wachezaji Farouk Shikalo,Mustapha Seleman na David Molinga wataukosa mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers baada ya kukosa leseni kutoka shirikisho la soka barani Afrika (Caf) baada ya kuchelewa kukamilisha taratibu za usajili.

Yanga ambayo iliondoka jana kwenda Botswana kupitia Afrika Kusini iliwakosa wachezaji hao katika mechi ya awali iliyofanyika nchini na kupata matokeo ya sare ya mabao mojamoja ilitegemea kupata leseni hizo kwa ajili ya mechi ya pili nchini Botswana lakini imethibitishwa rasmi wachezaji hao hawatokuwepo

Msimu huu CAF iliweka madirisha matatu ya usajili, dirisha la kwanza lilifungwa Julai 10 ambapo timu zilisajili bila faini huku dirisha la pili likafungwa Julai 21 ambapo timu zilipaswa kusajili kwa kulipa faini ya dola 250 kwa kila mchezaji atakayeandikishwa.

Dirisha la tatu lilifungwa Julai 31 ambapo timu zilipaswa kulipa faini ya dola 500 kwa kila mchezaji aliyeandikishwa hivyo wachezaji wote walioandikishwa kwenye dirisha la tatu hawaruhusiwi kucheza raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa Shikalo, Molinga na Mustapha hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo dhidi ya Township Rollers japo kuitumikia Yanga kuanzia raundi inayofuata kama timu itafuzu.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala