Connect with us

Makala

Sheva Arejea Kwenye Ubora Wake

Kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Miraji Athumani ‘Sheva’ ameonekana kuanza kurejea kwenye ubora wake akitokea kwenye maumivu ya misuli yaliyomsababishia kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili ambapo maumivu hayo aliyapata akiwa Taifa Stars kikosi kilichokuwa kinashiriki Cecafa,Uganda.
Sheva alijiunga na Simba kwenye msimu huu akitokea Lipuli FC ya mkoani Iringa ambaye alianza na kasi kubwa ya kufunga mabao sita kabla ya kuumia.

 

Hivi karibuni Sheva alionekana akifanya program zote za mazoezi pamoja na nyota wakubwa wanaochezea ligi kuu Bara ambao ni Haruna Niyonzima, Juma Kaseja, Said Ndemla, Hassani Isihaka, Shaaban Kado na wachezaji wengine wanaochipukia kwenye ufukwe wa Sea Scape uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kumaliza kufanya program ya viungo, vikosi viwili viligawanywa na kucheza mechi, wakati mazoezi yakiendelea Sheva alionekana kupiga mashuti ya mbali huku akikokota mpira kwa kutumia miguu yote miwili.
Mechi hiyo ikiendelea, Sheva alifunga bao kwa shuti la umbali wa mita 18 ambalo halikudumu kwa mda baada ya Mnyarwanda, Haruna Niyonzima kusawazisha kwa kumchambua Kado ndani ya sita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala