Connect with us

Makala

Senzo Aachia Mikoba Simba

Tetesi zinaeleza kuwa ofisa mtendaji mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa siku ya Jana jioni alikabidhi ofisi na nyaraka za klabu hiyo kwa madai ya kuwa hakuwa akisikilizwa huku taarifa zingine zikieleza kuwa mkataba wake umeisha.

Pia  kuna kikao kimeendelea leo ambacho wamejadili kuhusu mbadala wake na nani atakaimu kwa wakati huu huku mchakato mwingine wa kutangaza ajira ukifuata hapo baadaye.

Bodi ya Simba Sc imejadili kuwa mtu atakayepatikana kukaimu nafasi hiyo kutoka ndani ya kikao hicho hapaswi kutoka kwenye bodi ya wakurugenzi  kwa maana kuwa asiwe mjumbe wa bodi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala