Connect with us

Makala

Samatta Aweka Rekodi Uefa

Mtanzania Mbwana Samatta ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya klabu bingwa barani ulaya wakati akiichezea timu yake ya KRC Genk dhidi ya Reddbull Salzburg ya nchini Australia.

Katika mchezo huo licha ya Genk kupoteza kwa mabao 5-2 nahodha huyo aliweka rekodi nyingine ya kuwa mtanzania wa kwanza kufunga goli katika michuano hiyo baada ya kufunga kwa kicha cha kuchumpa akimalizia krosi iliyochongwa kutokea winga ya kushoto.

Licha ya kupoteza mchezo huo kwa idadi kubwa ya magoli Genk walionekana kutoa ushindani japo ugeni katika michuano hiyo mikubwa barani ulaya ulikua kikwazo cha kufanya vizuri na sasa wanajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Napoli ya italia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala