Connect with us

Makala

Samatta Atua Tanzania Leo

Mbwana Samatta amewasili leo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi utakaochezwa Oktoba 11 Jumapili kabla ya kuendea wiki ya watani itakayochezwa 18 Octoba,2020 uwanja wa Mkapa.

Nahodha huyo wa kitanzania kwa sasa anakipiga ndani ya klabu ya Fenerbahce ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Uturuki na tayari amecheza mechi mbili akiwa ametupia mabao mawili.

Taifa Stars inayonolewa na kocha mkuu ,Etienne Ndayiragije iliangia kambini Oktoba 5 ikiwa tayari kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa Octoba 11.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala