Connect with us

Makala

Samatta Anukia Uturuki

Mshambualiaji wa kitanzania anayeichezea klabu ya Krc Genk ya Ubeligiji Mbwana Samatta anasakwa na klabu ya Galatasalay ya Uturuki ili kwenda kuiongezea makali safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Inaripotiwa kwamba maafisa wa klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya uturuki wapo nchini ubeligiji kujaribu kufanikisha uhamisho wa mchezaji huyo aliyejiunga na Genk akitokea Tp Mazembe ya Kongo.

Mshambuliaji huyo ameichezea Genk mechi 168 akifunga magoli 68 huku ikidaiwa ana ndoto kutua ligi kuu ya uingereza japo taarifa zinadai mpaka sasa hakuna ofa yeyote rasmi kutoka timu za uingereza ziliwasilishwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala