Connect with us

Makala

Samatta Aanza Na 2-1 Fenerbahce

Nahodha wa Tanzania aliyejiunga na klabu ya Uturuki,Fenerbahce kwa mkopo akitokea Aston Villa,Mbwana Samatta ameanza kufanya yake kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo mpya kwa kupachika mabao 2-1 dhidi ya Faith Karagumruk kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Licha ya kutumia dakika 84 uwanjani Sukru Saracoglu ,Samatta alitupia mabao hayo dakika ya 24 kwa pasi ya Caner Erkin huku bao la pili akilitupia dakika ya 68.
Nyota huyo mwenye miaka 27 ni mechi yake ya kwanza kuanza kikosi cha kwanza ambapo ile ya kwanza dhidi ya Galatasaray alianzia benchi na alicheza kwa dakika 25 na mechi kumalizika kwa suluhu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala