Connect with us

Makala

Sakho Aitwa Senegal

Nyota wa klabu ya Simba Sc  Pape Ousmane Sakho ameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 cha timu ya Taifa ya Senegal kinachonolewa na kocha Mkuu Aliou Cisse kwaajili ya mechi mbili za kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Msumbiji.

Staa huyo kinda anaungana na mastaa wa ulaya wanaounda safu ya ushambuliaji kuelekea kwenye mchezo huo ambao ni Sadio Mane (Bayern), Boulaye Dia (Salerntana), Habib Diallo (Strasbourg), Bamba Dieng (Lorient), Iliman Ndiaye (Sheffield Utd).

Hii ni mara ya kwanza kwa staa huyo kuitwa katika kikosi cha wakubwa hasa kuelekea kujiandaa na michuano mikubwa barani Afrika kwa ngazi za timu za Taifa.

Licha ya kuwa na kiwango kizuri chenye kupanda na kushuka kwa nyakati flani flani staa huyo ni mwenye kipaji na maarifa mengi hasa anapokua na mpira mguuni huku uwezo wake wa kukokota na kukimbia kwenye nafasi ukiwa juu.

Sakho ambaye sasa anatumikia msimu wake wa pili kunako klabu hiyo pia ni mshindi wa goli bora katika michuano ya Caf mwaka jana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala