Connect with us

Makala

Rwanda Waingia Psg

Nchi ya Rwanda imesaini mkataba na timu ya Psg ya nchini Ufaransa ili kupromoti utalii wa nchi hiyo kimataifa huku ikishirikisha mastaa wa timu hiyo kupitia kampeni ya tembelea Rwanda (Visit Rwanda).

Kampeni hiyo mara ya kwanza ilianza kusainiwa kati ya nchi hiyo na Arsenal ambapo inasemekana Rwanda ililipa klabu hiyo dola milioni 44  kwa mkataba wa miaka mitatu huku katika mwaka wa kwanza tu nchi hiyo imeingiza dola za kimarekani milioni 88.

Psg itapromote utalii na bidhaa za nchi hiyo huku bango la “Visit Rwanda”litatokea katika jezi za timu ya wanawake wa klabu hiyo na  kwenye mabango uwanjani.

Japo thamani halisi ya mkataba huyo haijajulikana lakini taarifa zinadai mkataba huo una thamani ya kati ya yuro milioni 6-8.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala