Connect with us

Makala

Ronaldo Matatani

Nyota  wa klabu ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo ameingia matatani baada ya polisi kuanza kuchunguza suala la kutocheza katika mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya mastaa wanaocheza ligi ya Korea Kusini.

Polisi nchini humo wanalazimika kuchunguza suala hilo baada ya mashabiki kufungua kesi ya ulaghai dhidi Ronaldo na Promota husika baada ya kuahidiwa kuwa nyota huyo atashiriki mchezo huo hivyo kuwafaanya mashabiki hao kununua tiketi kwa wingi.

Baadhi ya mashabiki wakishangilia mchezo huo huku wakiwa na picha za wachezaji wa Juventus huku mmoja akiwa na kinyago cha Ronaldo.

Inadaiwa kuwa Ronaldo licha ya kuwepo katika benchi la timu hiyo aligoma kucheza na kuwalazimu mashabiki kuvamia ofisi za muandaaji wa pambano hilo kudai fidia ya kutomuana Ronaldo akicheza kama walivyoahidiwa japo polisi walifanikiwa kuwadhibiti mashabiki hao na kuwataka kufungua kesi.

Mechi hiyo ya maandalizi ya msimu ilichezwa julai 26 mwaka huu ambapo wakati mchezo ukiendelea mashabiki walikua wakitaja jina la staa huyo mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara tano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala