Connect with us

Makala

Ratiba Kombe La Dunia Ipo Hivi

Ratiba ya fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazopigwa Qatar imetangazwa ,huku ikishuhudia mechi nne zikichezwa kwa siku na fainali yenyewe kufanyika wiki moja kabla ya sikukuu ya krismasi.

Michuano hiyo itaanza Novemba 21,2022 ambapo Dunia kwa mara ya kwanza itashuhudia Kombe la Dunia likifanyika kipindi cha baridi kwa nchi za ulaya.

Katika michuano hiyo mashabiki watashuhudia mechi nne kwa siku ikiwa ni kwa mara ya kwanza,ambapo mchezo wa kwanza utakuwa saa 7 mchana,wa pili saa 10 jioni,wa tatu saa 1;00 usiku na wa nne saa 4 usiku kwa saa za Qatar ambapo ni sawa tu na Afrika Mashariki.

Mechi za hatua ya makundi zitamalizika Desemba 2,huku raundi ya hatua ya 16 bora itafanyika kati ya 6-9 Desemba.

Hatua za robo fainali zinatarajiwa kufanyika Desemba 9-10 baada ya mapumziko ya siku tatu ya mashabiki huku nusu fainali kupigwa Desemba 13 na 14 mashabiki wakiwa na mzuka wa krismasi.

Fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia itafanyika Doha,Uwanja wa Lusail mnamo tarehe 18 Desemba saa 12;00jioni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala