Connect with us

Makala

Rashford Ampa Tano Jose Mourinho

Mshambuliaji wa Manchester United ,Marcus Rashford amesema alivumilia kipindi kigumu chini ya aliyekuwa meneja wa klabu hiyo ya Old Traford,Jose Mourinho na kufanikiwa kuwa mchezaji bora.

Mourinho alikuwa meneja wa Maanchester United kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 na kufanikiwa kutwaa taji la Europa na kombe la ligi(Carabao Cup) katika msimu wa wake wa kwanza akiwa Traford.

Rashford alipachika mabao 28 na kutoa pasi 20 chini ya meneja huyo kutoka nchini Ureno,ambaye hivi sasa ni meneja wa Tottenham Hotspurs.

Mshambuliaji huyo kutoka England alionesha kiwango kizuri chini ya Mourinho  na anashukukuru kwa uzoefu alioupata chini ya mreno huyo ambaye kwa sasa amepoteza mvuto.

Tangu Mourinho alipofungashiwa virago na nafasi yake kuchukuliwa na Ole gunner Solskjaer bado Rashford ameendelea kuwasha moto, amecheka na nyavu mara 19 katika mechi 31 na kushuka dimbani msimu huu akiwa na Man United .

Kama nyota huyo asingelipata majeraha ni dhahiri angekuwa kwenye kilele cha wafungaji bora kama Vardy,Auba na Aguero

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala