Connect with us

Makala

Ramadhani Hii,Ozil Amekuwa Msaada

Kiungo wa Arsenal,Mesut Ozil ameonyesha utu wa kuwajali wengine  baada ya hivi karibuni kutoa kiasi cha pauni 80,000 (sh milioni 231) kwa lengo la kuwasaidia waislamu ambao wameathirika na janga la virusi vya Corona katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.

Nyota huyo ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki atasaidia chakula kwa ajili ya Waislamu 16,000 kwa kipindi chote cha mwezi wa Ramadhan ulioanza April kwa  kusaidia kufuturisha maeneo magumu ya nchini Uturuki.

 

Ozil anapokea mkwanja mrefu ndani ya Arsenal , ambao ni pauni 350,000 pia amekuwa ni mtoaji mzuri kwani amekuwa akiwalisha watu 100,000 wasio na makazi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala