Connect with us

Makala

Puto Lamponza Lacazette

Arsenal wamepanga kumwadhibu vikali mshambuliaji, Alexandre Lacazette baada ya kupata ripoti kuwa nyota huyo ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa alipatikana akivuta gesi ya Nitrous Oxide maarufu kama ‘Laughing Gas’ iliyokuwa imejazwa ndani ya puto .

Gazeti la Daily Star nchini Uingereza lilichapishwa makala zenye picha zilizoonyesha Lacazette akiwa na puto yenye gesi hiyo mdomoni.

Ni wiki moja pekee imepita tangu Lacazette apatikane miongoni mwa wanasoka wengine wa Arsenal waliokiuka kanuni mpya za afya zinazodhibiti maambukizi dhidi ya virusi vya corona.

Lacazette pia  alionekana akiwa karibu sana na mwanamume mmoja aliyekuwa akimwoshea gari lake jijini London, Uingereza na kuvunja kanuni inayotaka mtu kudumisha umbali wa hadi mita mbili kati yake na mwingine .

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala